VIDEO: Nguo ya mpenzi wa Hamornize yazua kizaazaa Instagram ya Hamisa Mobeto

Muktasari:

Awali, Juma lokole aliandika kwenye mtandao wa Instagram ujumbe unaosomeka: “… Hatimaye Sarah kaungama na kumtaja aliyemvalisha…kwanini mnasema uongo wakati vya bure mnavitaka? Yule dada naye anatafuta pesa, Welcome Bongo nyoso Sarah don’t worry about Insta”

Wakati sakata la Hamisa Mobeto kudaiwa kupigwa na mama yake Diamond nyumbani kwake Madale, mwanamitindo huyo amelianzisha varangati kwenye ukurasa wa Jumalokle na kusababisha majibizano makali.
Awali, Juma lokole aliandika kwenye mtandao wa Instagram ujumbe unaosomeka: “… Hatimaye Sarah kaungama na kumtaja aliyemvalisha…kwanini mnasema uongo wakati vya bure mnavitaka? Yule dada naye anatafuta pesa, Welcome Bongo nyoso Sarah don’t worry about Insta”
Ndipo Hamisa akajibu: “Mbona unatumia nguvu sana kuharibu biashara yangu Juma…sasa mfano Sarah  anajuaje nguo imetoka wapi? Kama aliniomba nguo na nikampa?...Hata kwenye redkapeti nilisema imedizainiwa na fulani na imeshonwa kwetu…tofauti hapo ni nini? Au mlitaka dada wa watu asipate riziki? Au hamjazoea wabunifu wa nguo kufanya kazi sehemu moja? Na hata kwenye picha yangu ya hiyo nguo nimemtag…Halafu kama unataka tangaza vita, sijui bifu na mimi usihangaike kuzunguka, maana ni siku kadhaa sasa naona unatumia njia ndefu…
Wakati huohuo Sarah wa Hanornize alitupia picha yake aliyovaa hiyo nguo na kuandika: “Thanks” kisha akawatagi watu walioshiriki kumvisha hiyo nguo huku akimtaja Hamisa Mobeto.
Sinema iliendelea kwa Hamisa kujibu: “Looking like a bag of…” huku akiweka alama ya dola.
Sakata hilo limetokana na nguo aliyovaa Sarah wa Harmornize, kudai aliyemvalisha ni Hamisa Mobetto kutoka kwenye duka lake la nguo, lakini Juma na baadhi ya watu wengine wanadai kuwa Hamisa ameongopa kwa kudai kuwa anahusika na nguo hiyo.