Kiba atoa ya moyoni Lissu apone

Muktasari:

Mbunge huyo ambae amelazwa Nairobi, Kenya, Ali Kiba alitoa neno juu ya ishu ya mbunge Lissu ambaye ni moja ya mfuasi wa wimbo wake wa Seduce Me.

NAWEZA nikasema kwa mwaka huu mpaka unamalizika Ali Kiba hawezi kusahau mafanikio aliyopata kutokea wimbo wake wa Seduce Me ambapo ukiachana na kuweka rekodi kwa kutimiza watazamaji milioni 2 kwa masaa 38 na watu mbalimbali mashuhuri kutoa ya moyoni kuhusu wimbo huo na mmoja wapo alikuwa ni mbunge Tundu Lissu.
Mbunge huyo ambae amelazwa Nairobi, Kenya, Ali Kiba alitoa neno juu ya ishu ya mbunge Lissu ambaye ni moja ya mfuasi wa wimbo wake wa Seduce Me.
“Namuombea kwa Allah tu, aweze kupona na kurudi katika hali yake ya kawaida sababu ni mtu ambaye nilishangazwa sana na maoni yake juu ya wimbo wangu, hicho tu sina mengi ya kusema,”