Chege Chigunda atoa somo Mfungo wa Ramadhan

Muktasari:

Akizungumza na MCL Digital alisema kuwa kwa Bongo watu wanakuwa wanapoteza maadili ya dini kwa sababu siku hizi miezi hii ya Ramadhani imehamia Instgram kitu ambacho wengi wanakosea.

Dar es Salaam. Msanii wa Bongo Fleva, Chege Chigunda amefunguka dhidi ya watu wanaouhamishia mwezi wa Ramadhan katika mitandao ya kijamii.
Akizungumza na MCL Digital alisema kuwa kwa Bongo watu wanakuwa wanapoteza maadili ya dini kwa sababu siku hizi miezi hii ya Ramadhani imehamia Instgram kitu ambacho wengi wanakosea.
“Kufunga ni imani na kusali ni Imani. Mimi nimefunga kwa kuwa kinachofunga ni imani yangu na roho, tusimuigizie Mungu tuwe wakweli tusifanye kwa kumuogopa fulani,” alisema Chege