Birdman kuja Tanzania mwakani

Muktasari:

Katika post yake hiyo aliyoweka katika ukurasa wake Instagram, Birdmad ambaye kwa siku za karibuni amengia katika mzozo na Lil Wayne amezitaja nchi kadhaa za Afrika anazotegemea kutembelea mwakani kuanzia Februari.

Dar es Salaam. Bosi wa lebo ya Cash Money, Birdman kupitia ukurasa wake wa Instagram amethibitisha mwakani mpango wake wa kutembelea Tanzania.
Katika post yake hiyo aliyoweka katika ukurasa wake Instagram, Birdmad ambaye kwa siku za karibuni amengia katika mzozo na Lil Wayne amezitaja nchi kadhaa za Afrika anazotegemea kutembelea mwakani kuanzia Februari.
Ukiachana na Tanzania pia amezitaja nchi nyingine za Nigeria, Kenya, Gambia na Ghana.
Kuja kwa rapa huyu kutaendeleza orodha ya watu mashuhuri mbalimbali waliotembelea Tanzania wakiwamo mcheza filamu Cynthia Rothrock, Sanje Dutt, Harrison Ford pamoja na wakali wengine kama Beckam waliotembelea vivutio mbalimbali vinavyopatikana nchini