Yanga yatinga robo fainali FA

Muktasari:

Jaffary Mohamed aliifungia Majimaji bao la kwanza dakika ya 60 dhidi ya Yanga, na kufanya matokeo kuwa 1-2 Yanga.

Songea. Timu ya Yanga imetinga hatua ya robo fainali kwenye mashindano ya Kombe la Shirikisho baada ya kuifunga Majimaji FC mabao 2-1 kwenye Uwanja wa Majimaji Songea leo Jumapili.
Pius Buswita aliifungia Yanga bao la kuongoza dakika ya 40 huku Emmanuel Martin akifunga bao la pili dakika ya 57 na kuwafanya mashabiki waliokuwapo uwanjani hapo kulipuka kwa shangwe.
Jaffary Mohamed aliifungia Majimaji bao la kwanza dakika ya 60 dhidi ya Yanga, na kufanya matokeo kuwa 1-2 Yanga.
Kwa ushindi huo, Yanga imefuzu kuingia hatua ya robo fainali ya michuano ya Kombe la FA ikiungana na timu za Njombe Mji, Azam FC, Singida United na Mtibwa Sugar.