TP Mazembe, MC Alger vitani Afrika

Muktasari:

Michezo ya leo ya Kundi B: Mjini Lobamba, Swaziland kutakuwa na debi ya kusini mwa Afrika kati Mbabane Swallows watakuwa wenyeji wa Platinum Stars ya Afrika Kusini, wakati debi ya kaskazini mwa Afrika itawakutanisha MC Alger watakaokuwa wenyeji wa CS Sfaxien jijini Algiers.

Cairo, Misri. Vumbi la mashindano ya Kombe la Shirikisho Afrika linaendelea leo na kesho kwenye viwanja mbalimbali barani Afrika.

Michezo ya leo ya Kundi B: Mjini Lobamba, Swaziland kutakuwa na debi ya kusini mwa Afrika kati Mbabane Swallows watakuwa wenyeji wa Platinum Stars ya Afrika Kusini, wakati debi ya kaskazini mwa Afrika itawakutanisha MC Alger watakaokuwa wenyeji wa CS Sfaxien jijini Algiers.

Nayo CF Mounana itakuwa mwenyeji wa SuperSport United, wakati Uganda wenyeji KCCA watakuwa na kibarua dhidi ya Club Africain ya Tunisia jijini Kampala.

Kesho mechi ya mapema itawakutanisha miamba ya Nigeria, Rivers United dhidi ya  FUS Rabat katika Kundi A, huku Horoya itawavaa TP Mazembe na Smouha dhidi ya Recreativo Libolo katika Kundi D na C.

Miamba ya Sudan, Al-Hilal Al-Ubayyid watakuwa wenyeji wa mabingwa wa Zambia, Zesco United.

Ratiba

Leo, Jumanne

Mbabane Swallows v Platinum Stars - Kundi B

CF Mounana v SuperSport United - Kundi  D

KCCA v Club Africain - Kundi  A

MC Alger v CS Sfaxien - Kundi  B

Kesho, Jumatano

Rivers United v FUS Rabat - Kundi  A

Horoya v TP Mazembe - Kundi  D

Smouha v Recreativo Libolo - Kundi  C

Al-Hilal  v Zesco United - Kundi C