Stars yataka heshima kwa Botswana

Muktasari:

Akizungumza na wanahabari makao mkuu ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Mayanga alisema wachezaji wanamorali ya hali ya juu.

Dar es Salaam. Kocha wa Taifa Stars,  Salum Mayanga amesema kikosi chake kipo fiti tayari kwa mchezo wa kesho dhidi ya Botswana.
Akizungumza na wanahabari makao mkuu ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Mayanga alisema wachezaji wanamorali ya hali ya juu.
"Wachezaji wote wako vizuri kiafya ya akili mpaka kimwili, tunataka kutumia mechi hizi za kirafiki  kama njia ya kutusogeza kwenye viwango vya Fifa," anasema Mayanga ambaye ni mechi yake ya kwanza tangu alipochukua jukumu hilo.

Nahodha wa Stars,  Mbwana Samatta amesema mechi hizo mbili za kirafiki watakazo cheza ni njia ya kuanza safari mpya ya kufanya vizuri.

"Huu ni mwanzo wa kuanza kurejea kwenye viwango vya juu,  hivyo tunakusudia kuanza kwa ushindi hapo kesho," anasema Samatta.

Kocha wa Botswana, Peter Butler wametamba amekuja kutafuta ushindi kwenye mchezo huo wa kirafiki.

Tayari TFF limetoa punguzo la bei ya viingilio kwenye mchezo huo ambapo bei ya mzunguko ni Sh. 3000 badala ya 5000 ya awali.