Snake Junior kurudi ulingoni

Tuesday April 18 2017

 

By Imani Makongoro, Mwananchi imakongoro@mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Bondia Mohamed Matumla Jr (Snake Junior) ametoa msimamo wake kwenye masumbwi na kueleza atarejea upya ulingoni 2019.

Matumla Jr, ambaye sasa afya yake imeanza kuimarika baada ya kuumia kwenye pambano la Februari 5 mwaka huu dhidi ya Mfaume Mfaume alisema hajastaafu kupigana.

 "Nimeambiwa nikae nje ya ulingo kwa miezi 12, lakini mimi sitapigana hadi 2019 ndipo nitarejea tena kwenye ngumi," alisema bondia huyo jana alipokuwa akizungumza na gazeti hili