Simbu atua London na matumaini kibao

Muktasari:

Simbu amesema amefanikiwa salama na anatarajia kufanya makubwa kwa ajili ya heshima ya nchi yake sambamba na kufuta ukame wa medali katika mashindano makubwa duniani. 

Arusha. Mwanariadha Alphonce Felix Simbu (24) amefika salama London tayari kwa kuiwakilisha Tanzania katika mashindano ya London marathoni yatakayofanyika Jumapili

Simbu amesema amefanikiwa salama na anatarajia kufanya makubwa kwa ajili ya heshima ya nchi yake sambamba na kufuta ukame wa medali katika mashindano makubwa duniani. 

ìHuu mwaka ni mwaka wa medali tu, Watanzania wafahamu sikuja London kushiriki wala kushangaa bali kushinda hivyo wajiandae na kupokea medali,î 

alisema Simbu na kuongeza kuwa anataka kutumia mashindano hayo katika maandalizi yake ya kuelekea katika mbio za duniani zitakazofanyika London, Agosti 

Katibu mkuu wa shirikisho la riadha nchini Wilhelm Gidabuday alisema Simbu ameondoka akiwa na matumaini makubwa ya kurejea na ubingwa hivyo ni faraja kwao pia.