Sakho aibua utata Liverpool

Mamadou Sakho

Muktasari:

BEKI wa kati wa Liverpool, Mamadou Sakho ameibua utata kuhusu hatima yake katika klabu ya Liverpool.

CALIFORNIA MAREKANI. BEKI wa kati wa Liverpool, Mamadou Sakho ameibua utata kuhusu hatima yake katika klabu ya Liverpool.

Hali hiyo imekuja baada ya kocha wa Liverpool, Jurgen Klopp kuamua kumuondoa katika orodha ya wachezaji wake walio Marekani kwenye ziara ya mandalizi ya kuukaribisha msimu mpya wa 2016/17.

Beki huyo wa kimataifa wa Ufaransa alitarajiwa kuwasili Uingereza Jumanne hii baada ya Klopp kuamua kumuondoa katika ziara hiyo.

Sakho anatarajia kupata matibabu ya majeraha yanayomsumbua na ambayo yatamfanya akose mechi za mwanzo za msimu wa Ligi Kuu England.

Hata hivyo kumekuwa na hofu kuhusu majaliwa ya mchezaji huyo kutokana na mienendo yake wakati akiwa na klabu hiyo, California, Marekani huku ikidaiwa kuwa hiyo ndiyo sababu kubwa ya kurudishwa kwake Uingereza.

Hata hivyo maofisa wa Liverpool walikiri mchezaji huyo kurudishwa Uingereza lakini walikataa kuzungumzia sababu hasa za uamuzi huo.