Rais wa Bayern aanza kusaka vipaji

Muktasari:

Mabingwa hao wa Ligi Kuu ya Ujerumani (Bundesliga) wameingia sokoni kusaka wachezaji wa safu ya ulinzi, kiungo na ushambuliaji.


Ofisa Mtendaji Mkuu wa klabu ya Bayern Munich, Karl Heinze Rummenigge ametaja orodha ya wachezaji ambao kocha wa klabu hiyo, Carlo Ancelotti angependa kuwa nao msimu ujao.

Mabingwa hao wa Ligi Kuu ya Ujerumani (Bundesliga) wameingia sokoni kusaka wachezaji wa safu ya ulinzi, kiungo na ushambuliaji.

Kwa sasa Bayern ina pengo la wakongwe waliostaafu, Philipp Lahm na Xabi Alonso, pia inasaka nafasi ya kujaza nafasi za wakongwe, Arjen Robben na Francky Ribery, ambao umri umeanza kuwatupa mkono.

Miongoni mwa nyota wanaotajwa ni mshambuliaji wa Arsenal, Alexis Sanchez  na kiungo  Marco Verratti wa klabu ya Paris Saint Germain (PSG).

Tayari, Bayern imewapa mikataba baadhi ya wachezaji wazawa, Sebastian Rudy na Niklas Sule,  ambao waliiwezesha Hoffenheim kumaliza kwenye nafasi ya nne na kukata tiketi ya Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu ujao.

Mbali ya Sanchez, Verratti, pia klabu hiyo inahusishwa na kiungo wa Schalke 04, Leon Goretzka, 22, pia mchezaji wa zamani wa Arsenal, Serge Gnabry pamoja na Julian Brandt. 

“Tuna nafasi kwenye  kikosi chetu ambazo lazima tuzijaze. Ni uamuzi ambao lazima utatuweka  sokoni,” alisema Rummenigge, ambaye alitamba kwenye kikosi cha Bayern na Ujerumani wakati wa ujana wake.

Akizungumza na mtandao wa klabu hiyo, alisema, “Tayari tumezungumzia masuala ya uhamisho, tumeangalia sera yetu ya uhamisho na usajili, kocha Carlo [Ancelotti] ameafiki na kuamua kuingia