Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Nyambui yaani wala hana mpango kabisa

KAMA bado unafirikia nyota wa zamani wa riadha aliyewahi kuwa Katibu Mkuu wa chama cha mchezo huo nchini (RT) Suleiman Nyambui ana mpango wa kurudi nyumbani Tanzania toka Brunei, pole yako. Nyambui alisema hana mpango huo.

Nyambui amefichua kuwa maisha anayo ishia katika nc hi hi yo ndogo, lakini tajiri akitembele gari la kisasa, akiishia kama mfalme akiwa na ulinzi wa kutosha na mshahara mnono, kitu kinachomfanya aendelee kukomaa nchini humo.

Alisema harudi kwa hivi karibuni kwani amekubalika na tayari wamemwomba aongeze mkataba mwingine wa miaka miwili baada ya ule wa awali wa miaka miwili pia kumalizika Juni 28 mwaka huu.

“Nimepata mafanikio kweli huku, wamenikubali na kunifanya nijione wa tofauti, wameniomba niongeze mkataba mwingine, kuja Bongo tena sio leo,” alisema Nyambui ambaye ni kocha pekee Mtanzania mwenye sifa za kufundisha riadha nje ya nchi.

Nyambui alipata dili hilo mwaka juzi na kuamua kuutema Ukatibu Ukuu wa Shirikisho la Riadha Tanzania (RT).