Muuaji wa Yanga aigeukia Simba

Mbao walivyoiduwaza Yanga Kirumba.

Mwanza. Mshambuliaji wa Mbao, Habib Haji aliyeifunga Yanga bao la kideo amesema sasa akili yake ni kuhakikisha anawafunga Simba katika fainali ya Kombe la Shirikisho la Azam itakayopigwa Jumamosi hii kwenye Uwanja wa Jamhuri, Dodoma.

Haji alifunga bao maridadi  katika mchezo dhidi ya Yanga mwishoni mwa wiki kwa kuwalamba chenga mabeki kabla ya kupiga shuti lililokwenda moja kwa moja wavuni.

Haji alisema akili yake kwa sasa ni kuhakikisha anafunga mabao katika mchezo wao wa Fainali ya Kombe la FA dhidi ya Simba.

Alisema mchezo huo ni muhimu kwao kuweka historia hapa nchini kwani wanataka kunyakuwa kombe hilo kwa mara ya kwanza.

“Akili yangu kwa sasa ni kujipanga kufunga bao katika mchezo ujao na Simba na kama nikifunga nitafurahi na nitapambana kuhakikisha natimiza haya malengo,”alisema Haji.