Msuva umekuwaje?

Saturday January 7 2017

 

WINGA machachari wa Yanga, Saimon Msuva ameweka rekodi ya kuwa mchezaji wa kwanza kukosa mkwaju wa penalti katika mashindano ya Kombe la Mapinduzi.

Msuva alikosa mkwaju huo dhidi ya timu ya Zimamoto ambao ulikuwa ndiyo mkwaju wa kwanza kutolewa katika michuano hiyo.

Straika wa Jang’ombe Boys, Abdul-Samad Kassim alifunga mkwaju wa pili wa penalti kutolewa katika michuano hiyo. Mpaka sasa ni mikwaju miwili ya penalti tu imetolewa katika michuano hiyo.