Msuva, Chirwa, Kaseke wafungiwa

Muktasari:

Wachezaji hao walifanya kitendo wakati wa mechi hiyo dhidi ya Mbao FC iliyofanyika Mei 20, 2017 kwenye Uwanja wa CCM Kirumba jijni Mwanza. Uamuzi wa Kamati umezingatia Kanuni ya 9(5) ya Ligi Kuu.

Dar es Salaam. Wachezaji wa Yanga, Simon Msuva, Deus Kaseke na Obrey Chirwa  wamesimamishwa kucheza mechi za Ligi Kuu wakati wakisubiri suala lao la kumsukuma na kumwangusha Mwamuzi Ludovic Charles kusikilizwa na kutolewa uamuzi na Kamati ya Nidhamu ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF). 

Wachezaji hao walifanya kitendo wakati wa mechi hiyo dhidi ya Mbao FC iliyofanyika Mei 20, 2017 kwenye Uwanja wa CCM Kirumba jijni Mwanza. Uamuzi wa Kamati umezingatia Kanuni ya 9(5) ya Ligi Kuu.

Mwamuzi Charles amepewa onyo kali kwa kutodhibiti vizuri mchezo.

 Uamuzi dhidi yake ni kwa mujibu w Kanuni ya 38(5) ya Ligi Kuu kuhusu Udhibiti wa Waamuzi.

Endapo adhabu hiyo itaendelea au itaongezwa basi Msuva, Kaseke na Chirwa kuna uwezekano mkubwa wa kukosa mechi za Ligi Kuu mwanzo wa msimu ujao.