Mshika kibendera gumzo Brazil

Wednesday April 19 2017

 

By Sao Paulo, Brazil

Mshika kibendera wa kike, Denise Bueno amezua balaa katika mechi ya soka ya wanaume kutokana na kulowa kwa fulana yake.

Mwanamitindo huyo, Bueno alijikuta akitolewa macho na midume wakati akichezesha mechi ya soka ya mashindano yasiyo ya ligi nchini Brazil kati ya timu za Desire na Sporting. 

Akiwa amevalia fulana iliyombana bila kuwa na brazia ndani, Bueno alifanya wachezaji kushindwa kuwa makini katika picha ya pamoja na kubaki wakimwangalia jinsi kifua chake kilivyokuwa kikionekana.

Wachezaji wawili katika kila timu walishindwa kabisa kumwangalia mpigapicha, huku wengine wakionekana kuwa na nyuso za matamanio zaidi ya paka aliyeona mnofu.

Baada ya hapo, Buenoalirudi uwanjani kuendelea na kazi yake, wakati fulana yake nyepesi ikizidi kulowa jasho na kufanya kifua chake kuonekana kirahisi kwa jasho.

 

Huo ulikuwa wakati mgumu kwa wachezaji 'wakware', ambao mara kadhaa macho yao yalikuwa juu ya kifua cha mwamuzi huyo wa pembeni.


Si mara ya kwanza kwa Bueno kufanya kituko hicho katika soka, kwani hata mpinzani wake katika masuala ya uremo, mshindi wa mashindano ya Miss Bum Bum, Suzy Cortez alikuwa akifanya hivyo na kupandisha picha zake katika mitandao ya kijamii.