Mpigambizi wa Taifa aanza kazi

Tuesday April 18 2017

 

By Imani Makongoro, Mwananchi imakongoro@mwananchi.co.tz


Dar es Salaam. Mwogeleaji wa timu ya taifa, Hilal Hemed Hilal ameanza mazoezi ya mwaka mmoja kwenye kituo cha kimataifa cha kuogelea cha Thanyapura nchini Thailand huku akipigia hesabu ya medali kwenye michezo ya Jumuiya ya Madola ya mwakani nchini Australia.

 

Hilal aliondoka nchini juzi baada ya Shirikisho la Kuogelea la Kimataifa (Fina) kumpa ofa ya mafunzo ya mwaka mmoja kutokana na kuwa mwogeleaji pekee wa Tanzania aliyefanya vizuri kwenye michezo ya Olimpiki ya Rio 2016, nchini Brazil.