Matumla Jr atoka hospitali

Muktasari:

Ofisa Habari wa MOI, Patrick Mvungi amesema,"tulimfanyia upasuaji wa kichwa baada ya kuumia mchezoni. Tumejiridhisha kwamba afya yake imetengamaa vizuri.

Dar es Salaam. Bondia Mohamedi Matumla (30) aliyefanyiwa upasuaji wa kichwa hivi karibuni katika Taasisi ya Mifupa MOI ameruhusiwa kurudi nyumbani leo.
Ofisa Habari wa MOI, Patrick Mvungi amesema,"tulimfanyia upasuaji wa kichwa baada ya kuumia mchezoni. Tumejiridhisha kwamba afya yake imetengamaa vizuri.
Aidha, tutaendelea kumfuatilia katika kliniki zetu, ili afya yake iendelee kuimarika zaidi," alisema Mvungi.
Matumla Jr alipatwa na mkasa huo baada ya kupigwa kwa Knockout (KO), alipondoka chini na kupata maumivu makali ya kichwa wakati wa pambano lake dhidi bondia Mfaume Mfaume.