Man City yampiga bei Hart

Muktasari:

Pep Guardiola inajulikana anataka kuona kipa huyo mwenye miaka 29, akiendelea kucheza nje ya nchini au kuumuza.
Lakini kwa mujibu wa Times, linadai kuwa Mhispania huyo yuko tayari kuuza Hart katika klabu yoyote ya England itakayofikia dau la pauni 20milioni.

Manchester City wapo tayari kumwachia kipa wake Joe Hart kwa klabu yoyote itakayofikisha dau la pauni 20milioni.
Kipa huyo wa England kwa sasa anacheza kwa mkopo Italia katika timu ya Torino, lakini atarejea Etihad mwisho wa msimu huu.
Pep Guardiola inajulikana anataka kuona kipa huyo mwenye miaka 29, akiendelea kucheza nje ya nchini au kuumuza.
Lakini kwa mujibu wa Times, linadai kuwa Mhispania huyo yuko tayari kuuza Hart katika klabu yoyote ya England itakayofikia dau la pauni 20milioni.
Torino walikuwa na matumaini ya kumchukua moja kwa moja Hart baada ya kuonyesha kiwango kizuri katika Serie A msimu huu, lakini dau la Man City litakuwa gumu kwao kumnunua.
Hata hivyo taarifa hiyo itakuwa nje kwa kocha wa Liverpool, Jurgen Klopp ambaye amekuwa akimfuatilia Hart kwa muda mrefu kwa lengo la kumsajili msimu huu.