Kipa wa Big G achemka kwa Mavugo

Muktasari:

Rostand ambaye kimwonekano ni mrefu wa futi sita na umbo kubwa lililojazia kwa mazoezi, alikuwa kikwazo kwenye ngome yake kutokana na kuokoa michomo hatari lakini dakika 57 Mrundi huyo aliyesajiliwa na Simba akitokea VitalO ya Burundi akazima ndoto zake na kufanya matokeo kuwa bao 1-0.

BAO la kiufundi lililofungwa na Mrundi Laudit Mavugo limemfanya kipa wa African Lyon, Mcameroon Youth Rostand atafute jina lake. Rostand ambaye kimwonekano ni mrefu wa futi sita na umbo kubwa lililojazia kwa mazoezi, alikuwa kikwazo kwenye ngome yake kutokana na kuokoa michomo hatari lakini dakika 57 Mrundi huyo aliyesajiliwa na Simba akitokea VitalO ya Burundi akazima ndoto zake na kufanya matokeo kuwa bao 1-0.

“Aliyetufunga kwenye FA anastahili pongezi, ni shujaa, alitumia mbinu akafunga, hakuwa na papara, alitumia akili na juhudi hakukata tamaa, mwingine asingeweza,”alisema Rostand na kuongeza: ‘‘Nafanya sana mazoezi ndiyo maana najiamini niwapo golini, mengine yanayotokea ni hali ya mchezo.’’ Bao hilo la Mavugo limewafanya Lyon waage mashindano ya FA, Simba wakitua robo fainali.

 

ATAFUNA BIG ‘G DAKIKA 90

Kipa huyo alitumia dakika 90 za mchezo huo akitafuna Big G amesema, alifanya hivyo ili kumwongezea kujiamini: “Mechi ilikuwa na ushindan, Simba timu kubwa, ina mashabiki wengi, hivyo ninapotafuna ile inanifanya niwe na furaha.