Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Jamaa wanampigia hesabu Ngoma

Muktasari:

Akizungumza na Mwanaspoti, Abdullman alisema: “Yanga ni wazuri wanacheza kitimu kuanzia nyuma hadi mbele, lakini yule straika mrefu namba 11 (Ngoma) aliyeingia kipindi cha pili alikuwa mzuri zaidi.

NAHODHA na beki wa MC Alger, Hachoud Abdullman ameweka wazi dakika 35 alizocheza straika Mzimbabwe Donaldo Ngoma ziliwaweka katika wakati mgumu na ndiye mchezaji wanayemhofia zaidi hata katika mechi ya marudiano wikiendi ijayo.

Abdullman, ambaye ana mwili wa kujazia na katika mchezo huo alivaa jezi namba 27 amesema, Yanga ni timu nzuri lakini waliimarika zaidi baada ya kuingia mchezaji huyo dakika ya 55 akichukua nafasi ya Deus Kaseke.

Akizungumza na Mwanaspoti, Abdullman alisema: “Yanga ni wazuri wanacheza kitimu kuanzia nyuma hadi mbele, lakini yule straika mrefu namba 11 (Ngoma) aliyeingia kipindi cha pili alikuwa mzuri zaidi. Ni mshambuliaji, ambaye ana uwezo wa kucheza mipira yote, ana nguvu na ndiyo maana alipoingia wakapata bao. Tumemwona hivyo tunarudi kwenda kujiandaa na mchezo wa marudiano kuona tunafanya vizuri,” alisema Abdullman.