Griezmann ataka dau zaidi kubaki Atletico

Muktasari:

Sakata hilo huenda likachochoa safari ya mchezaji hiyo kuhamia Manchester United. Jana Alhamisi taarifa iliyotolewa na uongozi wa klabu hiyo ilieleza kwamba hawana haja ya kumuachia nyota huyo kwenda klabu yoyote kwa sasa.

Madrid, Hispania. Sinema ya uhamisho wa mchezaji nyota wa Atletico Madrid, Antoine Griezmann imeingia hatua nyingine, baada ya uongozi wa klabu hiyo kugoma kumlipa mshahara wa Pauni 10 milioni kwa mwaka.

Sakata hilo huenda likachochoa safari ya mchezaji hiyo kuhamia Manchester United. Jana Alhamisi taarifa iliyotolewa na uongozi wa klabu hiyo ilieleza kwamba hawana haja ya kumuachia nyota huyo kwenda klabu yoyote kwa sasa.

Klabu ya Atletico imekuwa kwenye makubaliano na mchezaji huyo, huku wakitoa msimamo kwamba hawawezi kumlipa zaidi ya kiwango hicho.

Makubaliano hayo yameanza kufanyika ikiwa ni mbinu za kumzuia mchezaji huyo kuhusu uhamisho wake kwenda Manchester United.

Mchezaji huyo mwenye miaka 26, inasemekana iwapo atahamia Manchester United mshahara wake utakuwa Pauni 14 milioni kwa mwaka.