Fainali ya Man United, Ajax ulinzi wa kufa mtu

Muktasari:

Mchezo huo utawakutanisha Manchester United na Ajax huku kukiwa na hofu baada ya shambulizi la jana Jumatatu na kuua watu 22 katika Jiji la Manchester.

London, England. Shirikisho la Soka Ulaya (Uefa) limetangaza kwamba limeimarisha ulinzi kwenye mechi ya fainali ya Ligi ya Europa inayotarajiwa kufanyika kesho Jumatano.

Mchezo huo utawakutanisha Manchester United na Ajax huku kukiwa na hofu baada ya shambulizi la jana Jumatatu na kuua watu 22 katika Jiji la Manchester.

Takribani watu 59 walijeruhiwa wakiwamo watoto kwenye shambulizi hilo lililotokewa kwenye tamasha jijini Manchester, huku vyombo vya usalama vikithibitisha kutokea tukio hilo.

Polisi walifika eneo la tukio na kuwasaidia majeruhi. Pia Mkuu wa Usalama, Kamanda Ian Hopkins alithibitisha mtuhumiwa wa mauaji huyo aliuawa  kwenye eneo la tukia baada ya kusababisha mlipuko.

Tukio hilo limetokea ikiwa yamebaki masaa kadhaa klabu ya Machester United kukutana na Ajax kwenye fainali ya Ligi ya Europa jijini Stockholm Sweden.

Uefa imewahikikishia mashabiki wake  ambao walipanga kushuhudia mchezo huo, kufanya hivyo kwa sababu  usalama umeimarisha.

 “Tumeimarisha usalama kwenye fainali ya Europa. Hakuna mtu au kikundi cha wau kitakwamisha shughuli kwenye Stockholm labda wafanye kuvizia kwa mashambulizi,” ilisomeka taarifa ya shirikisho hilo la soka barani Ulaya.

Awali, Uefa walituma taarifa kwenye mtandao wao wa Tweeter wakielezea kushtusha na tukio hilo, huku wakisema wanaungana na familia za waathirika wote.

Rais wa Uefa, Aleksander Ceferin alitoa salamu zake za pole akisema,” Nimesikitishwa na tukio hili la ajabu la mashambulizi jijini Manchester. Imenishtua kutokana na kuuawa watu wasio na hatia. Ninawapa pole wanafamilia wote waliopatwa na athari kwa namna yoyote.”