Chambua: Huyu Chirwa vipi?

Friday April 14 2017

 

By GIFT MACHA

NYOTA wa zamani wa Yanga, Sekilojo Chambua, amesema kwa namna timu hiyo ilivyomvumilia,  straika  Obrey Chirwa, hakupaswa kugoma kusafiri kisa tu madai ya mishahara.

Chirwa alijiunga na Yanga mwezi Juni mwaka jana na kukutana na ugumu mkubwa hasa baada ya kushindwa kufunga kwa miezi minne mfululizo kitendo ambacho kilimfanya kuwa katika presha kubwa klabuni hapo.

Chambua alisema Chirwa alikuwa kwenye kiwango kibovu katika miezi yake ya mwanzoni Jangwani, lakini mashabiki na viongozi walimvumilia mpaka alipoweza kufunga kwenye mchezo dhidi ya Mtibwa Sugar mwezi Oktoba mwaka jana.

“Mashabiki na viongozi walimvumilia sana katika miezi yake ya mwanzo, alikuwa na kiwango kibovu sana. Mashabiki walimpa sapoti mpaka akafunga,” alisema.

“Amejichonganisha na mashabiki sasa, ikitokea ameshindwa kufanya vizuri atakuwa amejiweka pabaya, hakuna atakayeweza kumwelewa tena,” alieleza.

“Alipaswa kujali na maslahi ya klabu pia.”