Babi atabiri bao la Yanga

Muktasari:

  • Babi ambaye kwa sasa yupo Kisiwani Zanzibar na kikosi chake cha Jang'ombe amesema hayo ikiwa ni tahadhari kabla ya kuchezwa mechi hiyo.

Kiungo wa zamani wa Yanga, Abdi Kassim 'Babi' ametabili bao la Yanga litafungwa na mabeki wa kati.

Simba na Yanga zitacheza kesho mechi ya marudiano ya Ligi Kuu Bara kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Babi amesema na mabeki hao atakayefunga ni kati ya Nadir Haroub' Cannavaro' na Kelvin Yondani 'Vidic' na litakuwa la kichwa.

Babi ambaye kwa sasa yupo Kisiwani Zanzibar na kikosi chake cha Jang'ombe amesema hayo ikiwa ni tahadhari kabla ya kuchezwa mechi hiyo.

"Unajua siyo kama napendelea, lakini mechi ya Simba na Yanga kwa kawaida haina ufundi na mimi siyo mtabili, lakini kila ninavyoangalia naona kama Yanga wanashinda,"alisema Babi ambaye pia alishaichezea Yanga miaka ya nyuma.

"Tena ushindi huo utatokea nyuma kwa mabeki kama siyo Cannavaro basi litakuwa kwa Yondani mwisho mtaamini maneno yangu."

Hata hivyo, Babi amesema pamoja na utabili wake, atafanya kila linalowezekana kuhakikishe utabili wake anaushuhudia kwa macho Uwanja wa Taifa.