Wanavuna mkwanja mrefu nje ya uwanja

Muktasari:

Ukiachana na umiliki wa magari ya kifahari na mahekalu makubwa, lakini wanasoka hawa wana uwekezaji wa kutisha nje ya maisha ya soka, ambapo wanaingiza mkwanja wa hatari ili kujihakikishia kula bata na familia zao hata baada ya kustaafu soka.

MAISHA ya kila siku ya wanasoka wakubwa duniani yamegubikwa na mambo mengi kwelikweli. Yapo yanayofurahisha na mengine yanashangaza mno. Kama utaamua kuyaiga unaweza kuonekana kituko mbele ya jamii kwani, umaarufu walionao na fedha ndefu wanazovuna vinaweza kukupoteza.
Ndiyo wanaoongoza kwa starehe zote, kumiliki nyumba na magari ya kifahari na wanapoamua kula bata wakati wa mapumzikoni, unaweza kusema hakuna kesho.
Ukiachana na umiliki wa magari ya kifahari na mahekalu makubwa, lakini wanasoka hawa wana uwekezaji wa kutisha nje ya maisha ya soka, ambapo wanaingiza mkwanja wa hatari ili kujihakikishia kula bata na familia zao hata baada ya kustaafu soka.
Kwa bahati mbaya sana, wanasoka wengi kwenye ligi zetu nyumbani wameshindwa kufahamu kuwa kuna maisha baada ya soka hivyo, kuanza kujipanga mapema. Wengi huishia kuwa ombaomba baada ya kutundika daluga. Angalia mastaa wanaopiga mkwanja mrefu nje ya uwanja.

CLARENCE SEEDORF- UHOLANZI
Bado anatajwa kuwa kiungo mkabaji bora zaidi duniani akitamba kwa muda mrefu na AC Milan ya Italia. Kwa sasa ametundika daluga, lakini anapiga pesa ndefu kupitia umiliki wa mgahawa mkubwa wa vyakula vya Kijapani wa Finger’s.
Finger’s ambayo ni kampuni kubwa kwa sasa, inamiliki migahawa minne katika majiji ya Milan, Porto Ceryo na nyingine ikiwa Ufaransa na anajiandaa kufungua mwingine Dubai.
Mbali na kumiliki migahawa hiyo mikubwa, Seedorf kwa sasa ni Kocha wa Klabu ya Shenzhen ya China, ambako analipwa pesa ndefu na matajiri wa China waliogeukia soka.
Seedorf pia ni mchezaji aliyeweka rekodi ya kushinda taji la klabu bingwa Ulaya akiwa na klabu tofauti, Ajax, Real Madrid, Inter Milan na AC Milan.

GENNARO GATTUSO - ITALIA
Mpaka sasa hajatokea kiungo mkabaji mwenye roho ngumu na asiyechoka uwanjani na mbabe zaidi ya Roy Keane. Ndio alikuwa silaha ya AC Milan akishika eneo la kiungo ya chini.
Ana rekodi nyingi kwelikweli, lakini kabla ya kustaafu nje ya uwanja alikuwa akijihusisha na biashara ya maduka ya samaki kwenye Mji wa Gallarate.
Akiwa mtoto staa huyo alikuwa na ndoto ya kuwa mvuvi na hata alipoangukia kwenye soka aliamua kutimiza ndoto yake kwa kuuza samaki na kufungua maduka ya Gattuso and Bianchi Fish Shop.
Moja ya maduka hayo yalifunguliwa kwenye sherehe kubwa iliyohudhuriwa na Ronaldinho na David Beckham.
Gattuso ameshinda Kombe la Dunia (2006) na mataji ya Ulaya na Seria A.

ANDREY ARSHAVIN, RUSSIA
Ni mchezaji aliyeweka rekodi ya kuwa mchezaji ghali kusajiliwa na Arsenal ‘The Gunners’, pia anasifika zaidi kwa kupenda fani ya mitindo.
Andrey Arshavin ana shahada ya ubunifu wa mitindo, aliyoipata katika Chuo Kikuu cha St. Petersburg State University na kuachana na mafunzo ya kemia kutokana na kuingiliana na ratiba zake za mazoezi.
Arshavin (35), ambaye kwa sasa anaichezea Kairat ya Kazakhistan, alizindua lebo ya mavazi yake akitumia staili ya kushangilia kwa kuweka kidole mdomoni ambayo ni maarufu sana.

RIO FERDINAND - UINGEREZA
Aliweka rekodi ya kuwa beki ghali duniani wakati akinunuliwa kutoka Leeds United kwenda Menchester United mwaka 2000, ambayo iliitumikia kwa miaka 10.
Rio anamiliki jarida la 5 Magazine na mgahawa wa Rosso, ulioko katika mtaa maarufu wa mfalme, jijini Manchester huku pia akifanya kazi kama mchambuzi wa soka katika kituo cha BT Sport.
Ferdinand (37), kwa sasa anashuhulika na miradi ya kijamii chini ya taasisi ya ‘Rio Ferdinand Foundation’ inayolenga kutoa fursa ya elimu na ajira kwa vijana.
Aidha, Ferdinand aliyetwaa mataji saba ikiwemo taji la Klabu Bingwa Ulaya, Dunia na Ligi Kuu ya England akiwa na Man United, pia alihusika katika utengenezaji wa filamu ya ‘Dead Man Running’. Pia anamiliki lebo ya muziki ya White Chalk Music.

ERIC CANTONA- UFARANSA
Mungu wa Old Trafford ambaye jina lake lipo juu na linakumbukwa miaka yote. King Eric kwa sasa anajihusisha na filamu ambapo, moja ya kazi zake ni muvi ya Avatar.
‘King Eric alistaafu soka akiwa na miaka 30, aligeukia filamu na mpaka sasa ameshiriki zaidi ya 20, ikiwemo ya ‘Elizabeth’ aliyocheza mwaka 1998 akicheza kama Monsieur De Foix.
Kati ya filamu alizocheza ambazo zilimwingizia mamilioni ya fedha ni Looking for Eric, ambayo ni filamu pekee ambayo alitumia jina lake halisi.

DAVID BECKHAM - UINGEREZA
Anatazamwa na wanasoka wenzake kama kioo cha mafanikio nje ya uwanja, Beckham (41), ana miradi mingi inayomwingizia mkwanja mrefu ikiwemo mikataba ya udhamini aliyoingia na kampuni kubwa duniani. Kampuni kama Adidas, Armani, Samsung, Diet Coke, Burger King, Breitling, Pepsi na H & M zinamwingizia staa huyu wa Kiingereza fedha ndefu sana.
Kwa sasa ni mmoja wa wamiliki wa klabu ya Miami ambayo itaanza kushiriki MLS, alistaafu soka mwaka 2013, lakini anaingiza fedha mara mbili zaidi ya alichoingiza katika miaka yake 22 ya soka. Mwaka jana pato lake kwa mwaka lilikuwa ni dola 65 milioni.
Anamiliki kampuni za David Beckham Ventures Limited na Beckham Brand Holdings Limited, ambapo mkewe Victoria naye anavuna mkwanja wa kutisha kwenye fani ya mitindo.MAISHA ya kila siku ya wanasoka wakubwa duniani yamegubikwa na mambo mengi kwelikweli. Yapo yanayofurahisha na mengine yanashangaza mno. Kama utaamua kuyaiga unaweza kuonekana kituko mbele ya jamii kwani, umaarufu walionao na fedha ndefu wanazovuna vinaweza kukupoteza.

Anamiliki kampuni za David Beckham Ventures Limited na Beckham Brand Holdings Limited, ambapo mkewe Victoria naye anavuna mkwanja wa kutisha kwenye fani ya mitindo.