Singida Utd bado haijakata tamaa

ARUSHA. LICHA ya Singida United kuambulia sare ya bao 1-1 dhidi ya Kagera Sugar kwenye mwendelezo wa Ligi Kuu Bara juzi Jumamosi, bado uongozi wa timu hiyo  umesisitiza dhamira yao ya kutwaa ubingwa iko pale pale. 

Katibu Mkuu wa Singida, Abdulrahman Sima, alisema nafasi waliyopo mpaka sasa si mbaya na wanaendelea kupambania ubingwa.

Singida ipo nafasi ya nne na pointi 34, ikiwa ni alama nane nyuma ya Simba inayoongoza Ligi hiyo. Simba pia ina mchezo mmoja mkononi.

“Tumejikusanyia alama 34 katika michezo 19 na timu zote zilizokuwa juu yetu bado hatujakutana nazo kwenye mechi za raundi ya pili. Mechi dhidi yao ndizo zitatupa mwelekeo wa ligi hasa tutakapokutana nao na kupata matokeo mazuri,” alisema.