Mbao FC yapasuliwa Uwanja wa Kirumba

Muktasari:

Kichapo hiki ni cha pili kwa Mbao dhidi ya Singida United, kwani mzunguko wa kwanza ikiwa ugenini mkoani Singida, iliambulia kipondo cha mabao 2-1 na leo ikajikuta ikilala tena ikiwa nyumbani.

Mwanza. Mbao FC imeendelea kuwa wateja kwa Singida United baada ya kukubali kichapo cha mabao 2-1 kwenye mchezo wa Ligi Kuu uliopigwa leo Jumatano katika Uwanja wa CCM Kirumba Mwanza.

Mabao ya Batambuze dakika za nyongeza kipindi cha kwanza kwa mkwaju wa penalti na Kaseke dakika ya 59 yametosha kuizima Mbao ambayo iliambulia bao moja lililowekwa kimiani na Kyombo kwa mkwaju wa penalti dakika ya 51.
Licha ya kupambana kwa Mbao kutaka kusawazisha, ilijikuta ikishindwa kufurukuta kwa vijana wanaonolewa na Mholanzi, Hans Pluijm ambao walionekana kuwazidi uwezo wapinzani wake chini ya Mrundi, Ettiene Ndayiragije.
Kwa matokeo hayo, Mbao anabaki na pointi zake 18, huku Singida United wakifikisha alama 33 baada ya mechi 17 kwa kila timu.Saddam Sadick
Mwanza. Mbao FC imeendelea kuwa wateja kwa Singida United baada ya kukubali kichapo cha mabao 2-1 kwenye mchezo wa Ligi Kuu uliopigwa leo Jumatano katika Uwanja wa CCM Kirumba Mwanza.
Kichapo hiki ni cha pili kwa Mbao dhidi ya Singida United, kwani mzunguko wa kwanza ikiwa ugenini mkoani Singida, iliambulia kipondo cha mabao 2-1 na leo ikajikuta ikilala tena ikiwa nyumbani.
Mabao ya Batambuze dakika za nyongeza kipindi cha kwanza kwa mkwaju wa penalti na Kaseke dakika ya 59 yametosha kuizima Mbao ambayo iliambulia bao moja lililowekwa kimiani na Kyombo kwa mkwaju wa penalti dakika ya 51.
Licha ya kupambana kwa Mbao kutaka kusawazisha, ilijikuta ikishindwa kufurukuta kwa vijana wanaonolewa na Mholanzi, Hans Pluijm ambao walionekana kuwazidi uwezo wapinzani wake chini ya Mrundi, Ettiene Ndayiragije.
Kwa matokeo hayo, Mbao anabaki na pointi zake 18, huku Singida United wakifikisha alama 33 baada ya mechi 17 kwa kila timu.