VIDEO: Simba yajifua mikwaju ya penalti

Muktasari:

Katika mazoezi yao ya mwisho, Kocha Pierre Lechantre alionekana kusisitiza wachezaji wake wapige pasi za haraka ili waweze kupata bao.

Dar es Salaam. Klabu ya Simba imejifua kwa mara ya mwisho katika Uwanja wa Boko Veterani, wakijiandaa na mechi ya marudiano dhidi ya Al Masry, mchezo utakaopigwa nchini Misri.
Simba wanaenda katika mchezo huo huku wakiwa na kumbukumbu ya kutoka sare ya 2-2 kwenye mchezo wa kwanza uliopigwa katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Katika mazoezi yao ya mwisho, Kocha Pierre Lechantre alionekana kusisitiza wachezaji wake wapige pasi za haraka ili waweze kupata bao.

Lechatre alikuwa hataki kabisa kuweka mpira nyuma, mara kwa mara alikuwa akiwakomalia mabeki wake Erasti Nyoni na Mlipili wasikae na mipira nyuma, badala yake wawaishe mbele.