Niyonzima hatihati kukosa msimu wote

Muktasari:

Kiungo huyo wa Kimataifa wa Rwanda anasubuliwa ya majeruhi ya mara kwa mara tangu alipojiunga na Simba akitokea Yanga

Dar es Salaam. KIUNGO fundi wa Simba,  Haruna Niyonzima muda wowote kuanzia leo Ijumaa anaweza kupelekwa nchini India na kufanyiwa upasuaji wa mfupa uliokuwa juu ya mguu wa kulia ambao aliumia kabla ya kusajiliwa na Simba katika diisha kubwa.

Afisa habari wa Simba, Haji Manara alisema baada ya Haruna kufanyiwa vipimo aligundulika kuwa anashida katika mfupa wa juu uliokuwa katika mguu wake na anatakiwa kufanyiwa upasuaji ambao mpaka kuja kupona kabisa atakaa nje kuwa wiki tatu.

"Niyonzima muda wowowte atakwenda India na atakuwa huku kwa muda usiozidi siku tano na atafanyiwa upasuaji katika tatizo lake na kupata matatibu ambayo yatamfanya kukaa nje hadi mwishoni mwa mwezi machi na baada ya hapo ndio anaweza kuwa tayari kucheza," alisema.

Manara alisema wapinzani wao Gendarmerie ya nchini Djibouti watawasili usiku wa Jumamosi majira ya saa 7;30, na mgeni rasmi wa mechi hiyo atakuwa Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili Alhaj Ali Hassan Mwinyi, kabla ya mechi hiyo kutakuwa na burudani ya muziki kutoka kwa wasanii Bongo fleva.