Mikono ya De Gea gumzo Hispania

Muktasari:

Kipa huyo wa Man United amekuwa katika kiwango cha juu katika mchezo huo wa Ligi ya Mabingwa

Madrid, Hispania. Kipa wa Manchester United, David de Gea ameacha gumzo nchini Hispania, baada ya kucheza kwa kiwango bora mchezo wa jana usiku uliomalizika kwa suluhu dhidi ya Sevilla katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Umakini De Gea kusimama vyema kwenye milingoti mitatu, uliinusuru Man United kupoteza mchezo huo wa raundi ya kwanza wa hatua ya 16 bora.

Kipa huyo aliokoa michomo mingi ya washambuliaji wa Sevilla na ameacha historia kwa mashabiki wa soka Hispania.

Uwezo mkubwa aliyoonyesha mchezaji huyo katika mchezo huo, umeingiza katika rekodi ya kuwa ndiye kipa bora duniani.

De Gea mwenye miaka 27, siyo mzungumzaji na vyombo vya habari licha ya kuripotiwa taarifa anataka kujiunga na Real Madrid.

Sevilla ilitengeneza nafasi nzuri za kufunga, lakini kipa huyo aliuteka Uwanja wa Ramon Sanchez Pizjuan kwa umahiri wa kuokoa.

Mara ya kwanza aliokoa mpira wa kichwa uliopigwa na Steven N'Zonzi ambao kila mtazamaji aliamini lilikuwa bao  la kwanza Sevilla. Pia alikosa bao la Luis Muriel aliyekaribia kufunga.