Minziro kuifundisha KMC Ligi Kuu

Muktasari:

KMC imepanda daraja kucheza Ligi Kuu Bara msimu ujao pamoja na JKT Tanzania, Alliance School ya Mwanza, Biashara ya Mara, Coastal Union ya Tanga na African Lyon ya Dar es Salaam.

Uongozi wa KMC umemuhakikishia kibarua kocha wa timu hiyo Fred Felix Minziro na kumwambia ashindwe mwenyewe tu.
KMC imepanda daraja kucheza Ligi Kuu Bara msimu ujao pamoja na JKT Tanzania, Alliance School ya Mwanza, Biashara ya Mara, Coastal Union ya Tanga na African Lyon ya Dar es Salaam.
Minziro kocha wa zamani wa Yanga amekuwa na bahati mbaya ya kutimuliwa pale tu anapofanikiwa kuipandisha timu daraja hivyo wengi kudhani mambo yatakuwa hivyo hivyo hata kwa KMC.
Minziro msimu ulipita aliipandisha Singida United lakini baadae akatimuliwa na nafasi yake kuchukuliwa na Mholanzi Hans Pluijm akisaidiana na Jumanne Charle.
Mwenyekiti wa KMC, Suzane Massawe alisema hawana mpango wa kumuondoa Minziro kwani wanamuamini kuwa ni kocha mzuri.
"Tunamuamini Minziro ni kocha mzuri na wala hatuna mpango wa kumuondoa labda mwenyewe aamue kuondoka," alisema Suzane.
Suzane alisema mikakati yao ni kutafuta uwanja mzuri wa mazoezi kwa ajili ya maandalizi ya timu kwa msimu uajo wa ligi pamoja na kupata basi zuri la wachezaji.