Kidumu awapagawisha mashabiki hadi nguo kuchanika

Friday February 9 2018

 

By Na Rhobi Chacha

Zanzibar. Mwanamuziki Kidumu kutoka nchini Kenya ambaye kiasili ni mzaliwa Burundi, jana Alhamisi amepagawisha mashabiki katika Tamasha la Sauti za Busara hadi nguo yake kuchanika kwapani.

Msanii huyo ndiye mwanamuziki pekee  ambaye aliombwa na mashabiki kurudia kupanda jukwani mara mbili kutokana na kuwapagawisha kwa kuchanganya aina ya muziki.

Mkali huyo alipiga nyimbo zake na baadaye akapiga nyimbo za reggae za Bob Marey na Luck Dube.

Kidumu alipata mapokezi mazito ya mashabiki walioudhuruia katika tamasha hilo ikiwa ni mwaka mmoja tangu akosekane jukwaani.