Kapombe ajivunia ujasiri wake

Dar es Salaam. Beki wa Simba, Shomari Kapombe amesema mchezaji anayejitambua hawezi kuogopa kumshauri kocha anapoona kuna kitu hakiendi sawa.

Kapombe alimshauri kocha wake, Pierre Lechantre asimtoe Shiza Kichuya badala yake ametoe John Bocco aliyekuwa na maumivu ili aingie Laudit Mavugo wakati wa mchezo dhidi ya Al Masry jana.

"Nilikuwa nimewasiliana na Bocco, aliniambia mguu unamsumbua, ndio maana sikuona sababu ya kumtoa Kichuya aliyekuwa akisaidia timu," alisema Kapombe.

Hata hivyo; mashabiki wa Simba, walifurahishwa na kitendo cha Kapombe, kumkatalia kocha wake asimtoe Kichuya kwani tayari walishaanza kumzomea Mavugo wakati aanza kupasha misuri.