JKT Queens yaichakaza Alliance

Muktasari:

Hii ni mara ya kwanza kufanyika kwa Ligi Kuu ya Wanawake inayohusisha timu za kutoka katika mikoa mbalimbali

Dar es Salaam. JKT Queens imeanza kwa kishindo nane bora ya Ligi Kuu ya Wanawake kwa kuichapa Alliance Queens kwa mabao  4-0 katika mchezo uliofanyika kwenye Uwanja wa Meja Jenerali Michael Isamuhyo Mbweni, Dar es Salaam .

Wenyeji JKT Queens  walianza mchezo huo kwa kasi na kufanikiwa kupata bao la kuongoza lililofungwa na Fatuma  Mustapha kabla ya Donesia Daniel  kufunga  la  pili.

Wakati Alliance Queens akiendelea kushangaa Fatuma  Mustapha aliipatia JKT Queens  bao  la  tatu katika kipindi cha pili kabla ya mkongwe Asha Rashid kuhitimisha kalamu hiyo kw akufunga bao nne.

Kocha wa JKT Queens, Ali Ali alisema ushindi huo unawaongezea kujiamini katika mchezo wao wa pili dhidi ya Evergreen, utakaopigwa  Jumatano wiki hii.

Naye kocha wa Alliance, Ezekiel Chobanka alisema wachezaji wake alifanya makosa madogo madogo yaliyowagharimu, lakini watajipanga upya kwa mchezo ujao.