Diamond atinga mahakamani ndani ya Prado

Dar Es Salaam, Msanii wa Bongo Flevam Naseeb Abdul maarufu Diamond amewasili katika viunga vya Mahakama ya Hakimu Kisutu.

Diamond ambaye ameambatana mwanasheria wake, amewasili mahakamani hapa saa 5:30  asubuhi akiwa katika gari aina ya Land Cruiser Prado rangi ya bluu mpauko.

Mara baada ya kuwasili katika viunga vya Mahakama ya Kisutu alipitiliza moja kwa moja hadi Mahakama ya Watoto iliyopo ndani ya viunga vya Mahakama ya Kisutu.

Pia mwanamitindo, Hamisa Mobeto aliwasili mahakamani hapo na kuelekea kwenye eneo la Mahakama ya Watoto.