Dar Musica wahamishia majeshi Meeda

Monday January 8 2018

 

By RHOBI CHACHA

Dar es Salaam. Mwanamuziki Jado FFU na bendi yake ya  Dar Musica Original walikonga nyoyo za mashabiki wake waliojitokeza usiku wa kuamkia jana, kwenye Ukumbi wa Meeda uliopo Sinza Mori.

Shangwe na miruzi vilisikika kutoka kwa mashabiki kutokana na kukubaliwa ombi hili,ambapo pia Jado FFU aliweza kumpandisha jukwaani aliyekuwa rais wa FM Academia, Nyoshi El Saadat aliwasalimia mashabiki kwani muda mrefu hajaonekana kwenye jukwaa  kutokana na kuwa chimbo  akifanya mazoezi ya bendi yake mpya inayoitwa Bogos.

Bendi hiyo ni mara ya kwanza kufanya onyesho katika ukumbi huo ili konga nyoyo za mashabiki wake waliomba iwe inatumbuiza kila Jumapili katika ukumbi huo.

Kiongozi wa bendi hiyo FFU alikubaliana ombi hilo la mashabiki kuwa bendi hiyo itakuwa inapiga kila jumapili kuanzia saa 12 jioni hadi sita usiku.