Aisee! Kumbe mama alimtuma Telela

Muktasari:

Alisema, kama nina malengo ya kusoma na nataka kufanikiwa ni vizuri nikaondoka Dar es Salaam na kwenda Mtwara, ndio maana nikafanya hivyo.

KIUNGO wa Ndanda FC, Salum Telela ‘Shemeji’ aliamua kukimbia vyuo vyote vya Dar es Salaam na kwenda kusoma Chuo cha Uhasibu Mtwara baada ya kupewa ‘dili’ na mama yake mzazi.

Telela ambaye mwishoni mwa mwaka jana alimaliza masomo yake na kupata Shahada ya Uhasibu, amesema: “Nilikwenda kusoma Mtwara kwa sababu mama yangu mzazi aliniambia nifanye hivyo.

Alisema, kama nina malengo ya kusoma na nataka kufanikiwa ni vizuri nikaondoka Dar es Salaam na kwenda Mtwara, ndio maana nikafanya hivyo.

“Alisema, kama nitasoma hapa Dar es Salaam ni rahisi kudanganyika na kungekuwa na uwezekano mkubwa wa kutomaliza, lakini pia kule ni kwetu ndipo ilipo asili ya mama yangu.”

Telela ni kiungo aliyeichezea kwa mafanikio klabu ya Yanga miaka ya nyuma kabla ya kujiunga na Ndanda.