Simba, Yanga zarudishwa Taifa kwa masharti

Mkurugenzi wa Michezo nchini, Yusuf Singo

Muktasari:

Vigogo hao wa soka nchini wametakiwa kuutumia uwanja huo kwa mechi kubwa tu na si kila pam-bano lao.

SIMBA na Yanga hazijautumia Uwanja wa Taifa, tangu zilipovaana katika mechi yao ya Ngao ya Hisani Agosti 23, lakini sasa serikali imewarudisha kwenye uwanja huo kwa masharti maalumu.

Vigogo hao wa soka nchini wametakiwa kuutumia uwanja huo kwa mechi kubwa tu na si kila pam-bano lao. Mkurugenzi wa Michezo nchini, Yusuf Singo alisema: “Simba na Yanga zinaweza kurudi hapa sasa, ila kwenye mechi kubwa tu, hizo ndogo waendelee kucheza Uhuru.”Aidha Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Dk. Har-rison Mwakyembe alisema seri-kali haina presha na uchakavu wa Uwanja wa Taifa kwani ukarabati uliofanywa na Kampuni ya SportPe-sa utauweka kwenye hali nzuri hadi mwaka 2027.Akizungumza baada ya kukabi-dhiwa uwanja huo, Mwakyembe alisema: “Hatuna presha tena na uwanja wetu kwani ukarabati ulio-fanywa na wenzetu wa SportPesa umetufanya ‘tupumue’, miaka 10 sio kitu kidogo uwanja wetu ukiende-lea kuwa katika ubora ule ule wa kimataifa, hiki ni kitu cha kujivunia.”Mkurugenzi wa Utawala na Utekelezaji wa SportPesa Tanzania, Tarimba Abbas, alisema ukara-bati walioufanya umegharimu Sh1.4 Bilioni.“Tumefanya ukarabati wa kisasa na haukuishia kwenye ‘pitch’ bali umefanyika uwanja mzima hadi kwenye vyumba vya kubadilishia nguo ambavyo sasa vina muonekano wa kisasa zaidi,” alisema Tarimba.Simba na Yanga ndio wawakili-shi wa Tanzania katika michuano ya kimataifa mwakani, lakini pia zinashiriki Ligi Kuu Bara pamoja na Kombe la FA, hivyo ni wazi mechi baina yao ama na Azam ndizo zina-zoweza kupigwa Taifa kwa mashind-nao ya ndani.Kwa mashindano ya nje Yanga uwezekano wa kucheza hapo ni mkubwa pia.