Tathmini ya mchezo wa Yanga vs Njombe Mji kipindi cha kwanza

Muktasari:

Maeneo hayo ambayo Yanga imeyatumia zaidi ni eneo la upande wa kushoto na eneo lake la kati (kiungo) upande wa kulia ambao anacheza Raphael Daud na Hassan Kessy wanaonekana kucheza kwa kufanya majuku mengine na sio kushambulia.

Yanga imeonekana ikitumia zaidi  maeneo mawili kutengeneza mashambulizi yake huku Njombe nao wakionekana kuwa imara kwenye eneo lao la ulinzi.
Maeneo hayo ambayo Yanga imeyatumia zaidi ni eneo la upande wa kushoto na eneo lake la kati (kiungo) upande wa kulia ambao anacheza Raphael Daud na Hassan Kessy wanaonekana kucheza kwa kufanya majuku mengine na sio kushambulia.
Upande huo Daud anaonekana mara kwa mara akisogea ndani kwenye eneo la kiungo na Kessy haonekani akipanda kama ilivyokuwa kwenye michezo iliyopita, anacheza zaidi nyuma kuwasaidia ulinzi mabeki wa kati,Kelvin Yondani na Said Juma.
Pengine inaweza kuwa ndiyo mbinu  ambayo wameingia nayo kwenye mchezo wa leo.
Gadiel Michael na Emmanuel Martin wamekuwa na muunganiko mzuri kwenye eneo la kushoto,Papy Tshishimbi ndiye ambaye amekuwa akionekana zaidi kwenye eneo la kiungo la Yanga huku Maka Edward akikaba zaidi.
Ukabaji wa Njombe Mji hasa Yanga wanapokuwa kwenye eneo lao umewapa wakati mgumu Pius Buswita na Obrey Chirwa kufunga licha ya kupata nafasi kadhaa.
Njombe Mji imekosa mbinu za kupenya kwenye eneo la ulinzi la Yanga hivyo Ditram Nchimbi amekuwa akijaribu kwa kupiga mashuti.