Maguire atua United,aweka rekodi ya Dunia

Monday August 5 2019

 

By STANSLAUS KAYOMBO NA BRIAN CHARLES (TUDARCO)

BEKI Harry Maguire amekamilisha uhamisho wake wa Pauni 80 millioni akitua Manchester United na sasa akiweka rekodi ya kuwa mlinzi ghali zaidi duniani.
Beki huyo wa Kimataifa wa England atia saini katika mkataba wa miaka sita wenye kipengele cha kuongeza miezi mingine 12 zaidi.
Dili hilo lina thamani ya pauni 200,000 kwa wiki na mchezaji huyo mwene umri wa miaka 26 ameonesha kufurahia kujiunga na mashetani wekundu.
Maguire ameambia ukurasa wa klabu hiyo ,"ninafuraha kusaini katika klabu hii kubwa.Nimekua na maisha mazuri Leicester na ningependa kumshukulu kila mtu katika timu hile na mashabiki kwa ushilikiano mzuri walio nipa katika misimu yangu miwili,bila shaka Manchester united inapo fungua njia ,ni wakati muafaka.
 "Kutoka kwa mazungumzo yangu na meneja, nimefurahi juu ya maono na mipango aliyonayo kwa timu. Ni wazi kuona kuwa Ole anaunda timu kushinda mataji. Sasa ninatarajia kukutana na wachezaji wenzangu wa timu mpya na kuanza msimu. '
kocha wa Manchester united Ole Gunnar Solskjaer ameongeza;
"Harry ni mmoja wapo wa mabeki bora kwenye mchezo wa leo na ninafurahi kwamba tumeshika saini yake."

Advertisement