Yanga, Township Rollers mambo yameanza

Saturday August 10 2019

 

By Oliver Albert

KUMEKUCHA Taifa. Timu za Yanga na Township Rollers ya Botswana tayari zimewasili kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam tayari kwa mechi yao.
Township Rollers ya Botswana ndio waliokuwa wa kwanza kuwasili majira ya saa 10: 15 jioni ikitumia basi linalotumiwa na Azam ya hapa nchini.
Dakika tano baadae Yanga nao waliwasili na kuamsha shangwe kwa mashabiki waliokuwa nje ya Uwanja.
Timu hizo zitapambana kuanzia saa 12:00 jioni katika mchezo wa kwanza wa raundi ya awali yua Ligi ya Mabingwa Afrika.
Huo utakuwa ni michezo wa kulipa kisasi kwa Yanga baada ya mwaka jana kutolewa katika mashindano hayo na timu hiyo hiyo baada ya kukubali kipigo Cha mabao 2-1 kwenye Uwanja wa Taifa.
Yanga ilienda kulazimishwa suluhu ugenini na kuangukia kwenye playoff ya Kombe la Shirikisho Afrika kwa kuvaana na Welaita Dicha ya Ethiopia na kuing'oa na kufuzu makundi ya michuano hiyo kwa mara yao ya pili baada ya mwaka 2016.

Advertisement