Yamodo aibomoa Waruguru Bendi

Friday July 12 2019

 

By Rhobi Chacha

ALIYEKUWA mwimbaji na kiongozi wa bendi ya Saki Stars yenye maskani yake jijini Dodoma, Huessin Mohamed ‘Yamodo’ ameipa pigo bendi ya Waluguru baada ya kuwanyakua mpiga ngoma, Onesmo Victor na Paul pamoja na mcheza shoo Happy Onesmo.
Watatu hao waliokuwa tegemezi kwenye bendi hiyo yenye makazi yake mjini Morogorogo ambapo sasa wamejiunga rasmi na bendi mpya inayoitwa Gold Music chini ya mwanamuziki huyo, Yamodo.
Yamodo amesema lengo la kuwachukuwa wanamuziki hao ni kuwa na timu nzuri itakayofanya kazi bora kwa ajili ya kuwapa burudani mashabiki wa muziki wa dansi.
Yamodo anayetamba na wimbo wa Paranona amesema kutokana na ushindani wa bendi za Dodoma wamejipanga kuleta ladha ambayo wanaikosa mashabiki katika tungo za jukwaani.
“Nimejipanga vizuri sana hasa kuliteka soko la muziki jijini Dodoma, kuna bendi zipo na ni za miaka mingi lakini hazina ladha ambayo mashabiki wanahitaji hasa wenye tungo na burudani safi jukwaani," anasema
Yamodo ni muimbaji na mtunzi wa muziki wa dansi amewahi kutunga nyimbo kama Nimezaliwa peke yangu, Maisha bahati, Lawama za mapenzi, Laleyo, Nani kakudanganya, Pesa haina uzee,  Tikisiko la dunia, Kisa cha baba,  Penzi la dhoruba, Mama na  Paranona .

Advertisement