Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Ninja: Kocha akinihitaji nitakipiga Yanga

Muktasari:

Ninja alikuwa mmoja wa wachezaji muhimu wa Yanga katika idara ya ulinzi chini ya kocha Mwinyi Zahera ambaye kibarua chake kiliota nyasi kabla ya ujio wa Eymael.

BEKI wa kati, Abdallah Shaibu 'Ninja' ambaye alienda kufanya majaribio nchini Latvia katika klabu ya   FK Rigas ni miingoni mwa wachezaji wa Yanga, ambao wanafanya mazoezi kwenye Uwanja wa Chuo cha Sheria (Simu 2000) uliopo wilayani Ubungo jijini Dar es Salaam.

Ninja ambaye aliachana na Yanga mwaka jana baada ya kupata dili la kujiunga na MFK Vyskov ya Jamhuri Czech, amerejea nchini baada ya mambo kwenda ndivyo sivyo.

Beki huyo ambaye aliwahi kukichezea kikosi B cha LA Galaxy ya Marekani, amepokewa mikono miwili na uongozi pamoja na benchi la ufundi la Yanga ambalo linamwangalia chini ya kocha wao mkuu, Luc Eymael.

"Nipo hapa kwa mazoezi huku nikiseti mambo yangu sawa, kama kocha atapendezewa nami sitokuwa na sababu ya kukataa kuichezea Yanga kwa mara nyingine tena” amesema Ninja

"Siwezi kuweka wazi kila kitu ambacho kilikuwa kikiendelea nadhani ni muda wa kujipanga upya na kuona nawezaje kwenda tena nje na kujaribu," alisema nyota huyo ambaye aliwahi kutamba mitandaoni akiwa kwenye picha na nyota mkubwa duniani Zlatan Ibramovich.

Eymael ametoa nafasi kwa Ninja kujumuika na wachezaji wake kwa ajili ya mazoezi na inaelezwa kuwa kama atavutiwa naye huenda akawa sehemu ya kikosi chake kwa ajili ya msimu ujao wa 2020/21.

Inaelezwa kwamba kutokuwepo kwa maelewano ya karibu baina ya Ninja na waliokuwa wakimsimamia ni miongoni mwa mambo ambayo yalimfanya kuchukua maamuzi ya kukatisha naye mkataba na kurejea nchini.