Mgunda ajishtukia Coastal

Friday August 9 2019

 

By Charity James

KOCHA wa Coastal Union, Juma Mgunda amesema amesajili kikosi kulingana na uwezo wa klabu yao hawawezi kumsajili Meddie Kagere wakati uwezo wao ni mdogo.
Mgunda ameungana na kikosi chake leo akitokea katika timu ya Taifa akiwa kama kocha msaidizi chini ya Mrundi Etienne Ndayiragije ambaye anakaimu nafasi hiyo.
Alisema anashangazwa na wadau wa soka kubeza usajili wao huku wakiwa wanaelewa kabisa kuwa timu hiyo haina mdhamini ambaye anaweza kuwekeza hela kubwa itakayowafanya wasajili nyota yeyote wanaemtaka.
"Usajili tulioufanya unalingana na uwezo wa kipato kinachopatikana klabuni hivyo nina imani kwani ni mapewndekezo yangu mwenyewe tutakachokifanya kupitia nyota hao wanaowabeza kitawashangaza wengi," alisema.
"Usajili wangu umezingatia mahitaji kwa kiasi kikubwa kikosi changu kimevunjwa kwani kuna baadhi ya wachezaji nilikuwa nawategemea msimu ulioisha wameondoka hivyo nimeziba mabengo yao kwa kuzingatia," alisema.

Advertisement