Mbelgiji aushukia uongozi Yanga

Muktasari:

Eymael alijiunga na Yanga mwezi Januari mwaka huu akirithi mikoba iliyoachwa na Mwinyi Zahera aliyetimuliwa.

Kocha wa Yanga, Luc Eymael ameulaumu uongozi wa timu hiyo kwa kutomuwezesha kurejea nchini kutoka kwao Ubelgiji.
Eymael alisema licha ya juhudi kubwa anayofanya kuwasisitiza mabosi wake washughulikie suala la safari yake, bado hadi sasa hakijaeleweka.
Anasema kwa sasa anga la Ubelgiji limefunguliwa na baadhi ya ndege zimeshaanza kuingia na kutoka nchini humo baada ya kufungwa wiki kadhaa zilizopita ili kuchukua tahadhari za maambukizo ya virusi vya Corona.
"Baada ya kuona kimya katika makubaliano hayo niliwauliza tena GSM pamoja na
viongozi kwa nin i mpaka sasa bado sijatumiwa tiketi huku muda ukiwa unazidi kwenda
na mechi za Ligi Kuu Bara pamoja na kombe la Shirikisho la Azam, ratiba zake zimetoka
na zinakaribiwa kuchezwa.
Wote wawili walinipatia majibu kuwa ndege zimejaa jambo ambalo si la kweli, mimi nina watu wa mashirika ya ndege
tofauti ambao huwa nawasiliana nao mara kwa mara na walinieleza hivyo," alisema Eymael.
Eymael alisema kuwa jambo hilo limemsikitisha kwani makocha wa timu nyingine wameshawasili nchini/
Nimeendelea kuudhunika zaidi baada ya kuona picha katika mtandao kama makocha
wa Azam, ambao walikuwa huku Ulaya nao wameweza kurudi Tanzania kuendelea na
majukumu yao.
Kana kwamba hilo halitoshi baadhi ya wachezaji wa Simba waliokuwa nje
ya Tanzania nao wamefanyiwa utaratibu wa kurudi na tayari wameanza kazi.
Kimsingi jambo hili limenikwaza mno kwani nimeambiwa sababu zisizo na mashiko
huku siku zikiwa zinazidi kwenda na tunakaribia kucheza mechi za kimashindano bila
ya kuwepo na timu katika maandalizi kwa muda mrefu jambo ambalo naliona si afya
kwangu licha ya kwamba naendelea kuwasiliana na msaidizi wangu, Boniface Mkwasa
ambaye ndio anasimamia timu kwa wakati huu," aliongezea Eymael