Makambo akumbukwa Yanga

Muktasari:

Mwaisabula amesema hayo kabla ya mchezo wa Ligi ya Mabingwa wa Afrika kati ya Yanga na Zesco ya Zambia unaochezwa uwanja wa Taifa.

KOCHA wa zamani wa Yanga, Kennedy Mwaisabula amesema kikosi cha Yanga ili kusonga mbele wanatakiwa kutumia vizuri uwanja wa nyumbani.
Mwaisabula amesema hayo kabla ya mchezo wa Ligi ya Mabingwa wa Afrika kati ya Yanga na Zesco ya Zambia unaochezwa uwanja wa Taifa.
"Naona kosa kubwa ambao Yanga wanalifanya ni kushindwa kutumia nafasi nyingi za kufunga ambazo wamekuwa wakikosa mabao ya wazi,"
"Yanga kama wangekuwa na mchezaji Heritier Makambo zile nafasi za kufunga ambazo wanakosa angekuwa anafunga zaidi ya mbili,"
"Naona nafasi yake Makambo katika mechi hizi, lakini kukosekana kwake Yanga wanatakiwa kuwa tu makini kutumia nafasi hizo kufunga mabao kwani kwenye michezo hii ya Ligi ya Mabingwa Afrika ni ngumu kujirudia au kupata mara kwa mara,"
"Lakini wanatakiwa kutumia faidi hii ya wingi wa mashabiki waliojitokeza uwanja wa nyumbani kushinda ili mechi ya marudiano kule Zambia waende wakiwa na mtaji wao mkononi," alisema Mwaisabula.