Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kisa Morrison, Mabosi Yanga warukana

Muktasari:

Yanga baada ya kupata ushindi dhidi ya Singida United wa mabao 3-1 jana Julai 15, 2020 imepanda hadi nafasi ya pili kwenye msimamo wa Ligi Kuu Bara wakiwa katika mbio zakuhakikisha wanamaliza nafasi hiyo.

Kocha Eymael amefichua sarakasi zote zilizopo Yanga na hasa sakata la Morrison wanaopaswa kulitolea tamko ni uongozi wa klabu, lakini nao wakarudisha mpira kwa kocha huyo.

Mabosi wa Yanga kuanzia Makamu Mwenyekiti, Fredrick Mwakalebela na Ofisa Habari wa klabu hiyo, Hassan Bumbuli wote walisema muamuzi wa mwisho katika sula la Morrison ni kocha, lakini Eymael alisema wenye maamuzi ya mwisho ni uongozi kutoa adhabu kwa mchezaji huyo.

“Natakiwa kusema mchezaji nidhamu yake mbaya, lakini wenye jukumu ni wale wanaolipa mishahara, mimi natakiwa kuhakikisha timu inafanya vizuri. Klabu ndio inatakiwa izungumzie hili la Morrison na sio mimi, majukumu yangu ni kufundisha, kutoa vitamini, programu na mambo mengine,” alisema Eymael.

Kwa upande wake, Kaimu Katibu Mkuu, Simon Patrick alisema suala la nidhamu na mambo mengine ndani ya Yanga, bado hayajabaini na kama yapo hatua zitachukuliwa.

Lakini, kuhusu suala la Morrison alisema alishatoa maelekezo kwa Bumbuli (Ofisa Habari) ambaye naye alipotafutwa alisema kwa sasa nguvu na akili zipo katika mechi za Ligi zilizosalia.

“Ishu za Morrison tulishaachna nazo, tunawaza tufanye nini tumalize nafasi ya pili katika ligi,” alisema Bumbuli kwa ufupi.