Kina Aveva wakwama, ndugu wamwaga chozi

Friday September 20 2019

 

By Imani Makongoro

NDUGU, jamaa na rafiki wa aliyekuwa rais wa Simba, Evance Aveva na makamu wake, Godfrey Nyange 'Kaburu' wamemwaga chozi kwenye mahakama ya Kisutu baada ya Aveva na Kaburu kukosa dhamana kama walivyotarajia.
Ndugu hao waliangua vilio saa 14.50 baada ya hakimu kueleza kuahirisha kesi hiyo ambayo awali walitarajia wapewe dhamana.
Baada ya hakimu kuahirisha kesi hiyo hadi Jumatatu baadhi ya ndugu waliangua kilio huku wengine wakikaa vikundi wakijadiliana.

Advertisement