Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kidao: Hatuna tatizo na Amunike -VIDEO

Muktasari:

Amunike aliiongoza Taifa Stars kufuzu Fainali za Mataifa ya Afrika  mwaka huu ikiwa ni kwa mara ya kwanza tangu ilipofanya hivyo mwaka 1980.

SHIRIKISHO la Soka nchini (TFF) limesema halijapokea taarifa yoyote kutoka Shirikisho la Soka Duniani (FIFA) juu ya madai ya kocha wa zamani wa Taifa Stars, Emmanuel Amuneke raia wa Nigeria.


Akizungumza katika mkutano wa waandishi wa habari jijini leo Ijumaa, Katibu Mkuu wa TFF, Wilfred Kidao alikiri Amuneke kudai stahiki zake lakini FIFA haijawataarifu chochote kuhusu madai hayo.


"Mwalimu anatudai sehemu ndogo ya fedha za kusaini mkataba na bonasi baada ya kuiongoza kufuzu Fainali za Afcon.


"Kuhusu taarifa ya kutushitaki FIFA, binafsi kama suala hilo lingekuwepo, TFF ingeandikiwa barua kujulishwa lakini hadi sasa tunapozungumza FIFA hawajatuambia chochote juu ya jambo hilo.


"Kikubwa TFF kama taasisi tumejielekeza katika usimamizi mzuri wa masuala ya fedha, pia kuhakikisha hatuna madeni ndio maana tumelipa asilimia kubwa ya watu wanaotudai kwani lengo letu ni kufanya tuwe taasisi isiyodaiwa," alisema Kidao.


Kidao alisema Amuneke ambaye mkataba wake na TFF ulivunjwa Julai mwaka huu, alilipwa fedha za kuvunja mkataba huo na kwa sasa anadai kiasi kidogo cha fedha.